Jumatatu , 8th Jun , 2015

Msanii wa muziki Nuh Mziwanda, baada ya kuvuka kihunzi cha skendo ya kumpachika mimba binti, na kupelekea msukosuko katika penzi lake na Shilole, hatimaye ameongea na eNewz na kueleza mipango yake ya kuzaa mtoto na Shilole.

Nuh Mziwanda akiwa na mpenzi wake Shilole aka 'Shishi Baby'

Nuh ameileza eNewz kuwa, yeye pamoja na Shilole wanapenda sana kupata mtoto wao, ila anafahamu kuwa hiyo ni mipango ya Mungu na wakati wowote kutoka sasa ikitokea baraka hiyo watafurahi, huku akiweka mipango ya ndoa baada ya kutambulishana kwa wazazi.