Alhamisi , 22nd Jan , 2015

Muongozaji na prodyuza maarufu, Nisher ametua rasmi jijini Dar es Salaam akitokea mjini Arusha ambapo mwaka huu amejipanga vyema kufanya project maalum ya kutengeneza video kali za wasanii wa muziki Jijini Dar es Salaam.

Muongozaji na mtayarishaji video za wasanii wa muziki nchini Tanzania Nisher

Nisher ameilezea eNewz kuwa ujio wa project hiyo kubwa kabisa itawahusisha wasanii maarufu wakiwemo Fid Q, Ray C, Linah, Young Suma na wengineo wengi akisisitiza kuwa atawapa nafasi wasanii wengine wakubwa kufanya naye kazi.

Kwa sasa Nisher anaendelea kula matunda ya kazi zake ambazo zinatamba katika vituo mbalimbali vya luninga nchini ikiwemo video ya XO ya kundi la Weusi na video aliyoitengeneza iitwayo 13 aliyoimba Young Killer akiwa na Fid Q.