Jumatano , 25th Nov , 2015

Baghdad, rapa ambaye pia kwa sasa anatambulika kama Baba Kyle, mtoto ambaye amempata sambamba na kutoka kwa kazi yake mpya inayokwenda kwa jina 'Ninaye' Ft Nandy ambayo imepokelewa vyema na mashabiki.

Rapa Baghdad wa nchini Tanzania

Msanii huyo ameeleza kuwa kazi hiyo inaweka rekodi ya kufunguka kwa baraka na mashavu mengi kwa upande wake sasa, licha ya kuwa ni kazi ambayo alianza kuifanya miaka 2 iliyopita.

Baghdad amesema kuwa, pembeni ya kazi ya video ambayo ndio unaitazama sasa, kati ya mashavu aliyopata ikiwa kama ni baraka za ujio wa mtoto wake wa kiume ni kuwa sehemu ya mradi mkubwa wa lebo ya muziki ambayo imejikita katika kusaka vipaji katika sekta ya burudani na kuviendeleza.