Jumatatu , 14th Dec , 2015

Msanii mkongwe wa bongo fleva Squeezer amesimulia mkasa uliowahi kumtokea maishani mwake wa kujaribu kujiua, kwa kujirusha kwenye pantoni alipokuwa akivuka kwenda kigamboni jijini Dar es salaam.

Squeezer ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa sababu kubwa iliyompelekea kutaka kufanya hivyo ni pombe alizokunywa, ambazo alikuwa amezidisha kiwango.

“Nishawahi kulewa sana nikataka kuruka kwenye pantoni, nimetoka town kipindi hicho naishi kigamboni, nikawa nimekutana na rafiki zangu wamefurahi na mimi wengine walikuwa nje kwa muda mrefu, tukawa tumekutana sehemu tunakunywa kunywa, sa sijui ni furaha ilizidi nikapitiliza kiasi cha kunywa, nikafika kigamboni tuko kwenye pantoni inamove nikasema nataka kuruka, kweli nikataka kuanza kupanda kuna mtu akanizuia, nikasema that's stupid”, alisema Squeezer.

Pamoja na hayo Squeezer amewataka vijana kujituma na kuwaza vitu vitakavyowasaidia baadae, na pamoja na kujiingiza kwenye shughuli za kilimo, huku akisisitiza kuwa maisha hayana njia ya mkato, na yanataka kuwa na subira.

“Mi napenda kuwashauri vijana wenzangu hamna kitu kinakuja haraka, kwa hivyo wawe na na moyo wa subira lakini pia wawe na program zenye mazao yanayoonekana, hata ukifanya kilimo, ufugaji ni kitu simple alafu ni rahisi kumanage kilimo au ufugaji kwa sisi ma capital less fighter, tusiwe na tamaa maisha yanaenda taratibu hamna aliyezaliwa akawa rich”, alisema Squeezer.