Ijumaa , 25th Sep , 2015

Msanii Nikki Wa Pili, amesema ukuaji unao tafsiriwa sasa kwa mabadiliko yanayoendelea kwa upande wa sanaa ni kwa upande wa uzalishaji tu na sio faida kwa wasanii.

msanii wa muziki Nikki wa Pili

Nikki wa pili ambaye ni mchambuzi mahiri kutoka kundi la Weusi ameeleza kuwa, ukuaji huo wa sanaa umefaidisha wasanii wachache huku wengi wakikwama katika kipindi cha miaka 10, Ikilinganisha na vile sanaa yao ilivyotumika katika jamii.

Kuhusiana na kukua kwa sanaa hapa Bongo, hii ndio tathmini ya msanii huyu msomi Nikki.