Ijumaa , 16th Sep , 2016

Producer mkongwe kwenye game ya bongo fleva Master Jay, amesema amefurahishwa na EATV kuanzisha tuzo za muziki na filamu kwa wasanii wa Afrika Mashariki, na kusema ni watu sahihi kufanya hivyo.

Master Jay akiwa kwenye Planet Bongo ya EA Radio

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Master Jay amesema kwa muda mrefu alikuwa anatamani kitu kama hicho, kuona watu wanaoujua muziki na sanaa kiujumla wakiandaa tuzo kwa wasanii.

"Kwa muda mrefu mi nilikuwa nasema ukiwa unafanya tuzo za muziki, unatakiwa kudeal na watu wa media, iwe ni watu wa radio na Tv, hawa ndiyo watu wanaelewa soko lote la muziki, ikiwa ni video au audio, kwa hiyo mi nimefurahi sana kuona imeanzishwa na media house ambayo inalielewa soko letu, mna information za kutosha kwa ajili ya kutoa tuzo, mi nimefurahi sana na nina matumaini makubwa sana", alisema Master Jay.

Master Jay aliendelea kusema kuwa East Afriva Tv wanaujua muziki wa Afrika Mashariki na chimbuko lake, kwani umekuwa ukitoa 'suport' kubwa kwenye kuinua game la muziki huo, na bado ana imani kuwa kuna watu wanafanya vizuri, hivyo mwisho wa siku tunaangalia wasanii gani walifanya vizuri kwa hicho kipindi.

Tags: