Ijumaa , 29th Jun , 2018

Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Amri Athuman a.k.a Mzee Majuto amesema kuwa nyonga ndio tatizo kubwa linalomsumbua kwa sasa jambo ambalo linamfanya ashindwe kufanya kazi zake kama alivyokuwa hapo awali huku akidai endapo zitaachia basi ataweza kukimbia kama Ronaldo.

Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Amri Athuman a.k.a Mzee Majuto

Mzee Majuto amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuwepo tetesi nyingi za hivi karibuni kuzushiwa kuwa amefariki jambo ambalo amesema sio vibaya kwa mtu kufariki lakini sio vizuri kumsambazishia mtu uzushi usiokuwa na faida yoyote.

"Nyonga ndio inanisumbua yaani ikiashia tu ikakaa sawa sawa nitaweza kukimbia kama vile Ronaldo. Kutokana na tatizo hili la nyonga nimeshauriwa nifanye mazoezi madogo madogo nasio yale makubwa sana", amesema Majuto.

Pamoja na hayo, Majuto ameendelea kwa kusema "wale wote ambao wananiombea mabaya mimi siwezi kuwalaumu kwasababu Mwenyezi Mungu ametuumba katika hali tofauti lakini ninaomba kama nimewaudhi mimi basi mnisamehe nami pia nimewasamehe lakini mimi mzima sijafa ila nataka niwaambie tu kuwa kufa ni lazima hivyo tutakufa tu".

Mtazame hapa chini Mzee Majuto akifunguka mengine zaidi kuhusiana na kuacha sanaa ya maigizo pamoja na kusamehe pesa zote ambazo anazodai watu.