
Mzee Hashim Kambi
Hashim amesema kuwa, kutokana na hali halisi ya sasa ya wasambazaji kufaidika zaidi na kazi za sanaa kuliko wasanii wenyewe, kuungana kwao kutamaliza tatizo hili na vilevile kuiweka Afrika Mashariki katika ramani ya soko la filamu duniani kama ilivyo kwa Nigeria.
Mwigizaji huyu amezungumza haya katika uzinduzi wa umoja mpya wa wasanii kutoka nchi Tano za Afrika Mashariki kwa lengo la kutengeneza mfumo mpya wa uandaaji na usambazaji wa kazi zao.