Alhamisi , 2nd Nov , 2023

Mwanamuziki Mwasiti ametangaza kuzindua kampeni yake ya (Kipepeo Mweusi) ambayo ni program ya kuandaa wasanii wa kike na mabinti kuhusiana na kupinga ukatili,suala ya uchumi, afya na kuwajengea uwezo wa kuwa na uthubutu, utofauti, malengo na ndoto kubwa.

Picha ya Mwasiti, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Gerson Msigwa na Katibu wa BASATA Kedmon Mapana wakizindua Kipepeo Mweusi.

Mgeni rasmi wa tukio hilo la Mwasiti kuzindua Kipepeo Mweusi ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamuduni Sanaa na Michezo Gerson Msigwa Katibu Mtendaji wa BASATA Dkt Kedmon Mapana.