Jumapili , 8th Jan , 2023

Rais wa Manzese Madee amewataja wasanii wa HipHop Mwana Fa na Fid Q kuwa ndio rapa wake bora kwenye mziki wa BongoFleva kwa sababu HipHop yao inauza na wanajaza shows.

Picha ya msanii Mwana Fa kulia na Fid Q kushoto

"Nina sifa nyingi sana zakuwapa hawa watu wawili hawa ndio rappers bora toka kuanzishwa kwa mziki wa BongoFleva. Sijaona, sijamsikia, sijaambiwa kama kuna wa kuwazidi hawa jamaa wawili"

"Kuna viswahili vya aina mbili unavipata kwenye ngoma zao. Kuna kiswahili cha pwani na cha bara, hawa ndio wale HipHop yao inauza, hawa ndio wale rappers shows zao hua zinajaa" - ameandika Madee