Vijana vijana ambao wamenusurika kupata ajali kutokana na wimbo wa Darassa
Wimbo huo uliojizolea umaarufu na kusambaa karibu kila kona ya nchi, ulitaka kusababisha ajali baada ya dereva wa gari kutekwa na hisia na kujikuta anafanya uzembe na makosa ya barabarani baada ya dereva huyo kutoka katika usikani wa gari wakati gari ikitembea na kuanza kucheza ngoma hiyo ya muziki.
Baada ya kuona clip ya vijana hao msanii Darassa alionesha kutofurahia kitendo kilichofanywa na vijana hao lakini anakiri wazi kuwa hisia huenda ziliwateka na kujikuta wakifanya jambo ambalo huenda lingeweza kuleta madhara kwao au kwa mtu mwingine, lakini anawaombea akiamini kuwa kwa kufanya hivyo huenda wamejifunza kuwa wamefanya jambo ambalo halikuwa sawa.
Darassa
"Hawa ndugu zetu nimepata taarifa wamekamatwa kwa kosa la kutaka kusababisha ajali na unaweza kuona kama mchezo ulielekea kubaya, ingeweza kuwa tatizo kwao au kusababishia tatizo mtu mwingine. Nasikia watakuwa mahakamani leo 'I'm not so sure' naendelea kufuatilia na nawaombea tatizo hili Mungu awafanyie wepesi 'I'm sure wamejifunza hawawezi kufanya tena mistake kama hii itokee, mizuka 'feelings' mtu anaweza kufanya kitu nje ya mipango yake sometimes, Mungu awasaidie" aliandika Darassa
Tazama kipande cha video hiyo:-