Mwana HipHop huyo ameeleza hayo leo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
"Siwezi kudanganya natamani ningetokea Nigeria, jinsi upendo walionao kwa wasanii wao, jinsi wanavyodumisha tamaduni zao, asilimia 90 ya maudhui ya Redio na Tv zao, wanacheza muziki wao bila kujali wapo Duniani, Umoja waliokuwa nao kwenye soko la muziki ni ndoto tu!"
Pia msanii huyo ameendela kuandika kuwa anawapenda wasanii wa Nigeria walivyokuza muziki wao wa Afrobeats, na hajui tatizo ambalo linakwamisha nchi yake kutoendelea kimuziki labda chuki.
Msanii huyo ameandika hayo baada ya kuona muziki na wasanii wa Nigeria unakuwa kila siku na kuzidi kutanua wigo barani Africa na Duniani kwa Ujumla.
