Alhamisi , 24th Sep , 2015

Nyota wa kughani mashairi na muziki wa asili Mrisho Mpoto, ameweka wazi nafasi kubwa aliyoipata ya kutembelewa na kituo cha habari kikubwa cha kimataifa kutoka Marekani, baada ya kutambua mchango wake katika suala zima la utamaduni la lugha.

Nyota wa kughani mashairi na muziki wa asili Mrisho Mpoto

Mpoto amesema kuwa, ameweza kukaa na ugeni huo kwa wiki nzima wakifuatilia na kujifunza asili anayoiwakilisha kutoka hapa Tanzania, akitoa wito kwa wasanii wenzake pia na wasani, kuamini na kuwakilisha vilivyokuwa vya kwetu, ambapo inakuwa ni rahisi zaidi kuonekana nje ya mipaka tofauti na kuwakilisha vile vya kuiga.

Msanii huyo pia ametumia nafasi hii kutoa ujumbe kwa waislamu na watanzania wote kwa ujumla katika kusherekea siku ya Eid akiwataka kujikita katika ibada na kujiepusha na shari.