
Miss Uganda 2014 Leah Kalanguka
Uwepo wa Leah unatarajiwa kuongeza chachu kwa ushiriki wa vijana, ambapo mbali na riadha kutakuwa pia na shughuli nyingine za kisanaa, ili kunogesha zaidi siku hiyo, lengo likiwa ni kukutanisha watu wa rika mbalimbali hususan vijana, ili kuimarisha umoja wa nchi za eneo hilo la Afrika.
Mbio hizi kwa mwaka huu zinasonga na kaulimbiu “The East Africa I would like to live in.”, na washiriki wake watapata nafasi za kujishindia zawadi mbalimbali endapo watamaliza mbio katika nafasi ya kwanza.
