
Mesen hivi karibuni amesikika na kusema kuwa kuna watu wanashindwa kusapoti muziki na kuanza kuuponda ndio maana muziki hapa nchini haukui na kufika mbali kwa sababu wasanii wamejifunga sehemu moja kwa kusimamia misingi huku walioitengeneza misingi hiyo wanaibadilisha.
"Kwangu mimi watu ambao walikuwa wanaongea vibaya kuhusu wimbo wa kazi kazi uliokuwa na beat ya singeli ni kama wana mapungufu ya akili. Yaani kama kuna 'fuse' zimewatoka hivi, ndio maana muziki wetu haukui na hauendelei kwa sababu tunataka kujifungia sehemu moja-” alisema Mesen.
Aidha Mesen ameongeza kwamba hakutegemea kama wangetokea watu kumponda na kumwongelea vibaya rapa huyo kwa sababu hawakuwa wanajua nini tafsiri ya Profesa kufanya kazi ya singeli, na kuongeza kwamba muziki wa rap unaweza ukafanywa kwenye 'beat' yoyote na ndivyo wafanyavyo wasanii wote wakubwa duniani.
Professor J ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mikumi alijikuta matatizoni kwa kushambuliwa na kutukanwa mitandaoni kisa wimbo wa 'Kazi Kazi' aliomshirikisha Sholo Mwamba ambao kwa kiasi kikubwa ulifanya vizuri lakini watu walimponda kwa kudai ameshusha hadhi yake..