Picha ya msanii Meja Kunta
Kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram wa Wasowiso amepost picha ya Meja Kunta kisha ameandika "Habari zinazoendelea mitandao sio za ukweli Meja Kunta anaendelea vizuri mzima kabisa".
Aidha kwa upande wa meneja wa msanii huyo aitwaye G Maker, ambaye alitoa taarifa za kufariki kwa msanii huyo ameomba msamaha kwa kutoa taarifa hizo kupitia mtandao wa Instagram ambapo ameandika.
"Ndugu Watanzania, mashabiki wa mziki wa singeli na mziki kwa ujumla, Wazazi, Waandishi wa wa Habari, ndugu jamaa na marafiki, nasikitika au kuomba radhi kwa nilichokiandika jana usiku kupitia ukurasa wangu wa instagram, Meja Kunta ni mzima wa afya nipende kuwatoa hofu, naomba sababu ya post niiongelee wakati mwingine. kwa dhati kabsa naomba samahani tena" ameandika G Maker
Kupitia EATV & EA Radio Digital, Siku ya Jumamosi Februari 1, 2020, tuliripoti taarifa ya msanii huyo kupata ajali ya gari maeneo ya Segera, Tanga mida ya alfajiri wakati akitokea Dar es Salaam kwenda kufanya show mkoani humo.