Marioo aibuka na Albamu

Ijumaa , 16th Jul , 2021

Hitmaker wa "Mama Amina" na zingine kibao, Marioo ameweka wazi kuwa album yake itatoka mwezi wa 9 mwaka huu.

Marioo ame-share taarifa hizo njema kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa mwezi Septemba 25,2021 itakuwa ndio tarehe rasmi ya kuachia, ingawa hajaweka wazi jina wala idadi ya nyimbo na wasanii aliowashirikisha kwenye album hiyo.

Hii itakuwa ni album yake ya kwanza kwa nyota huyo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wake kwenye uimbaji na uandishi wa nyimbo zake.