Msanii Man Fongo
Man Fongo ametoa ufafanuzi huo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja, baada ya kuenea kwa tetesi kwamba msanii huyo kashindwa kulipa kodi na kuanza kuomba marafiki wake wa karibu wamsaidie huku akiirudisha familia yake nyumbani kwao.
"Huo ni uzushi na hizo taarifa hazina ukweli wowote, mimi naishi na familia yangu, na ndio baba wa familia. Nina ishi na mke wangu, watoto, dada zangu pamoja na kaka zangu pia", amesema Man Fongo.
Pamoja na hayo, Man Fongo ameendelea kwa kusema "katika maisha lazima uzungumziwe. Naweza kuwapeleka hata sasa hivi ninapoishi wengine wanaishi kwenye varanda mimi naishi kwenye nyumba kubwa, watu waache maneno".
Aidha, Man Fongo amedai haoni shida watu kumzungumzia kwasababu wanamfanya aishi na kuonyesha kuwa watu wanamfuatilia sana hivyo kwake haoni kama ni shida.
Man Fongo amekuwa ni miongoni wasioishiwa 'skendo' za hapa na pale juu ya muziki wake anaoufanya na kuutangaza vyema hadi kufikia kupata tuzo ya 'EATV AWARDS' katika kipengele cha msanii bora chipukizi kwa mwaka 2016.