Jumatatu , 7th Oct , 2024

Mama mzazi wa Diddy, Janice Combs amevunja ukimya matatizo yanayomkabili mtoto wake akisema hana hatia sababu Diddy hajafikia hatua ya kufanya unyama huo kwa watu wanaomtuhumu.

Picha ya Diddy na mama yake

Mama Diddy amemtetea mwanae kupitia barua ya wazi inayoeleza yanayoendelea kwa Diddy ni uongo na uchochezi kwa wanaotaka faida ya fedha.

"Mwanangu sio mnyama wanamchoresha kuwa hivyo, ni mzaha na kucheka maisha ya mwanangu yakiporomoka mbele ya macho yetu ni jambo ambalo siwezi kusahau kamwe".

"Inasikitisha kuona ulimwengu ukigeuka dhidi ya mwanangu juu ya uwongo na maoni potofu bila kusikia upande wake. Uongo huu unaotupwa huchochewa na wale wanaotafuta faida ya kifedha na sio haki" - Maeleozo ya Mama Diddy

Mpaka sasa Diddy anatuhumiwa makosa 120 ya madai ya unyanyasaji wa kingono.