
WIZ KID
Lufa amesema studio ya Swich Record ambayo inamilikiwa na msanii QUICK ROCKA ndiyo studio yake ya kwanza kufanya kazi na tayari amekwishatoa ngoma kali kibao ikiwemo watabamba na nyingine kibao ambazo zilishika chati kwenye stesheni za radio mbalimbali.
Hata hivyo Lufa kasema ana uwezo wa kutengeneza hadi biti tano kwa siku kwahiyo anakaribisha wasanii wa aina zote za muziki na gharama zake ni laki tano kwa wimbo mmoja na ndoto zake ni kufanya ngoma nyingi zaidi bila kuchagua ili kuweza kujitangaza kimataifa.