Antoine Christophe Agbepa Mumba a.k.a Koffi Olomide
Kofi ambaye jina lake halisi ni Antoine Christophe Agbepa Mumba atafanya onyesho hili akiwa sambamba na bendi yake nzima kwaajili ya kuwapatia wakenya burudani ya moja kwa moja ya muziki halisi wa Bendi.
Mkali huyu wa miondoko ya sokous aamejijengea sifa kubwa kutokana na uzoefu wake wa miaka mingi katika kuufanya muziki, kitu ambacho kinaongeza msisimko zaidi kwa mashabiki wake kuhusiana na ujio wake huu huko Kenya.