Jumatatu , 7th Apr , 2014

Baada ya Mamlaka ya Mapato ya nchini Uganda, URA kuachia gari ya msanii Jose Chameleone hivi karibuni, maelezo yametolewa kuwa msanii huyu alilazimika kulipa shilingi milioni 40 za Uganda, kiasi cha kodi zilizotokana na shoo alizofanya huko Uganda.

Jose Chameleone

Mamlaka hii imesema kuwa, wamekuwa wakiwasiliana na msanii huyu tangu mwezi Novemba mwaka jana ili kumtaka alipe deni lake la kodi, na baada ya kutoona majibu ya kuridhisha kutoka kwake, waliamua kulishikilia gari lake.

Msanii huyu kwa upande wake ameitaka mamlaka hii kuweka sheria zake katika lugha inayoeleweka zaidi ili kumfanya mlipa kodi kuona uhalali na umuhimu wa wajibu wake katika kulipa kodi.