Ijumaa , 25th Apr , 2014

Kesi ya msanii wa muziki wa nchiri Rwanda aliyewekwa kizuizini kwa mashitaka ya ugaidi, Kizito Mihigo pamoja na washirika wake, imeanza kusikilizwa ambapo wamesomewa mashtaka yao katika mahakama mjini Kacyiru, Rwanda.

Kizito Mihigo na watuhumiwa wenzake

Msanii huyu pamoja na wenzake, kutoka katika mahojiano ya awali, tayari wamekwisharipotiwa kukiri kuhusika na mipango ya kufanya vitendo vya kigaidi kwa madhumuni ya kupindua serikali, kitendo ambacho kinatarajiwa kurahisisha mchakato wa kesi hii.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka polisi kwa waandishi wa habari, washtakiwa hawa endapo watapatikana na hatia, watakabiliwa na kifungo cha miaka 15 mpaka 25 gerezani, kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo.