Ijumaa , 7th Mar , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Maurice Kirya ameweka wazi kuwa kwa sasa hayupo katika mahusiano ya kimapenzi kutokana na mpango wake wa kuelekeza nguvu zake zote katika kazi zake hususan muziki.

Maurice ambaye anafahamika zaidi kwa kuimba nyimbo za hisia hususan mapenzi, ameweka wazi haya katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni ambapo pia amefunguka kuwa, anamhusudu sana mwanadada Juliana Kanyomozi kutokana na muonekano na namna ambavyo anatupia akiwa kama msanii.

Maurice ambaye kwa sasa anatamba na albam mpya ya The Book of Kirya, amefichua kuwa, kando na suala la mahusiano, kujituma kwake katika muziki kumempatia mafanikio makubwa ikiwepo ziara katika nchi zaidi ya 35 na miji mikubwa 40 ndani ya Afrika na Ulaya, akiiwakilisha vyema Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla.