Ijumaa , 11th Dec , 2015

Staa wa muziki Matonya, ameweka bayana siri ya kuweza kukaa katika muziki kwa muda mrefu, wasanii wanaochipukia wakitakiwa kufahamu kuwa kipaji na heshima ndio mbinu za pekee za kumuwezesha msanii kuweza kuendelea kuwepo na kufanikiwa katika muziki.

Staa wa muziki nchini Matonya

Matonya amesema kuwa anaheshimu sana kazi ya muziki anayoifanya, na vilevile watu wanaomzunguka akifahamu kuwa binadamu ana mapungufu, na hapa na pale kuna umuhimu wa kuomba radhi na kujirekebisha pale makosa yanapotokea.