Mtangazaji wa East Africa TV King Smash
Taarifa hiyo iliripoti kuwa mtangazaji huyo anashea mahusiano na wanawake wawili tofauti na wanafanya kazi pamoja ambao ni Tina ripota wa show ya eNewz ya East Africa TV na Dolly Dolly mtangazaji wa The Base ya ITV.
King Smash amesema watu wanafuta 'content' za kuzungumziwa ili kujiingizia pesa kupitia yeye ila binafsi anaona suala hilo haliwezi kumshusha wala kumpandisha kwenye upande wake wa kazi.
"Sina 'comment' yoyote kuhusiana na hilo, mimi huwa sizungumzii ujinga pia siwezi kutolea ufafanuzi vitu vya kipuuzi na udaku, siwezi kukwazika wala kufurahi kwa kilichotokea kwani watu wanaingiza pesa kupitia mitandao ya kijamii wanatafuta 'content' kwa kuwazungumzia watu fulani ili wao wapate pesa hizo" amesema King Smash
Tumejaribu kuwatafuta wanawake wote wawili ili kuweza kufanunua suala hili kwa bahati mbaya hawakuweza kuonyesha ushirikiano wowote.
