Jumanne , 27th Mei , 2014

Ziara kubwa ya muziki ya Kili Music Tour, baada ya kuwarusha wakazi wa Moshi katika ufunguzi rasmi kwa namna ya aina yake, kwa sasa inaelekea Mwanza ambapo burudani nzima itadondoshwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Katika jukwaa sasa kikosi cha wakali kimekamilika kikiwa na Ommy Dimpoz, Izzo Business, Fid Q, Weusi, Ben Pol, Mwasiti, Dabo, Young Killer, Vanessa Mdee, Richard Mavocal pamoja na Christian Bella.

Itakuwa ni Burudani ya Bandika Bandua na shoo hii ya kiwango, kiingilio kitakuwa ni shilingi 2,500 tu na kama haitoshi utapatiwa bia yako moja ya Kilimanjaro mlangoni Bureee.

Mwanza hii ni ya kwetu, Kilimanjaro Music Tour 2014, Zungusha Kikwetu Kwetu.