Jumapili , 15th Dec , 2019

Toni-Ann Singh ni mrembo kutoka nchi ya Jamaica ambaye usiku wa kuamkia leo Disemba 15, 2019, ameitoa kimasomaso nchi yake mara baada ya kutwaa taji la Urembo wa Dunia katika mashindano ya kumsaka mlimbwende wa Dunia (Miss World), yaliyofanyika Jijini London, nchini Uingereza.

Mrembo wa Dunia 2019/2020 kutoka nchini Jamaica, Toni-Ann Singh.

Shindano hilo ambalo jana ilikuwa ni mara yake ya 69 kufanyika, lilikutanisha warembo kutoka Mataifa mbalimbali duniani, ambapo nchi ya Tanzania iliwakilishwa na Mrembo Sylvia Sebastian Bebwa, ambaye yeye kwa juma lililopita aliingia katika 20 bora ya warembo wenye vipaji, baada ya yeye kuonesha kipaji cha kucheza 'Robot Dance'.

Mbali na Urembo, Mlimbwende huyo wa Dunia anapenda kutoa Elimu ya afya ya akili na matarajio yake ni kuwa Daktari na taji lake amelipokea kutoka kwa Venessa Ponce De Leon, Mrembo kutoka nchini Mexico alitwaa taji hilo mwaka 2018.

Katika mashindano hayo mshindi wa pili alikuwa mrembo kutoka Ufaransa, Ophely Mezino, wa tatu ni Suman Rao kutokea nchini India