Jumamosi , 4th Apr , 2015

Wakati siku zikiendelea kusogea kuelekea tukio kubwa la Uchaguzi mkuu mwaka huu, Kampeni ya ZamuYako2015 imeendelea kushika kasi ikipata sapoti kubwa kutoka kwa wasanii.

Izzo Business

Rapa Izzo Business akiwa Miongoni mwao, amesema katika kipindi hiki cha pasaka ambapo atakuwa mkoani Mbeya, atazungumza na vijana kuwahamasisha kushiriki katika uchaguzi.

Izzo Business amesema kuwa, akiwa hafungamani na upande wowote, kwa maana ya vyama vya kisiasa, na akiwa anaelewa kuwa vijana wa Mbeya wana muamko na masuala ya kisiasa, atawasisitizia suala zima la umuhimu wa kura yao, sambamba na kudumisha amani katika kipindi kizima cha uchaguzi.

Izzo Business pia amesisitiza kuwa, vijana wanatakiwa kuelewa kuwa maamuzi ya mapinduzi ya maendeleo yao, kwa asilimia zote yanashikiliwa na maamuzi ya kumchagua kiongozi sahihi ambayo yote yanatokana na kupiga kura.