Waigizaji wa BongoMovie Irene Uwoya na Wema Sepetu.
Irene Uwoya amesema hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, kwenye hafla ya chakula cha usiku kati ya wasanii na waandishi wa habari, iliyofanyika siku ya Novemba 4 katika moja ya Hotel iliyopo Masaki, Jijini Dar es Salaam.
"Nataka niwaambie kwamba hichi ni kipindi ambacho tunaenda kufunga mwaka, lakini pia nitakuwa nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa ambayo itakuwa ni tarehe 18, kwahiyo kabla ya mwaka kufunga wasubiri kitu kizuri kutoka kwangu, kitu ambacho ningemwambia Wema Sepetu ni kufanya filamu moja ya mwaka" amesema Irene Uwoya.
Aidha staa huyo wa filamu ameendelea kusema "Siamini kama Wema amepoteza mvuto kwa sababu bado ni mzuri na anavutia,pia mahusiano yake na Aunty Ezekiel ni ya kawaida tu na ni watu ambao wa muda mrefu sana" ameongeza.
Pia amesema kuna haja ya mastaa kutenganisha maisha yao binafsi na mitandao ya kijamii ila kuna muda huwa inawabidi tu kuwaweka watu wao wa karibu au familia zao kama watoto au wapenzi.