Jumamosi , 3rd Oct , 2015

Rapa mkongwe wa Bongo Flava, Inspekta Haroun amesema kuwa licha ya wasanii wapya hususan wale wanaoimba kufanya vizuri katika soko la muziki sasa, wanahatarisha kupotea kwa alama halisi ama misingi iliyokuwepo katika Bongo Flava kutokana na kuigana.

Inspekta Haroun

Inspekta amesema kuwa, katika kipindi kilichopita wao kama wasanii walipigania kupata muziki ambao unakuwa na asili ya hapa hapa nyumbani, kitu ambacho hakizingatiwi tena na kusababisha wasanii wengi kufanana katika kile wanachofanya.