Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Hospitali wameiba dawa za kulevya - Sirro

Ijumaa , 26th Mei , 2017

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amefunguka kuwa wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala wameiba jumla ya kete 32 za dawa za kulevya zilizokuwa kwenye mwili wa raia wa Ghana aliyefariki dunia akiwa katika nyumba ya wageni.

Kamishna Simon Sirro

Kamanda Sirro amesema wahudumu hao wanne wote wamekamatwa na kukiri kwamba  baada ya kifo cha raia huyo wa Ghana aliyefariki ndani ya 'Red Carpet' iliyopo Sinza Dar es Salaam walipasua mwili wa raia huyo na kutoa kete hizo kisha kuziuza, na kuongeza wametaja watu ambao wamewauzia ambao nao wamekamatwa na wapo chini ya ulinzi wa polisi

"Yule Mghana ambaye alikutwa amefariki dunia tarehe 14/ 03/ 2017 kwenye nyumba ya wageni ya 'Red Carpet' na alichukuliwa na kupelekwa mochwari Mwananyamala lakini inaonekana wale wahudumu wali[pata taarifa kuwa ule mwili una dawa za kulevya, kimsingi walikula njama wakampasua na kutoa kete 32 za madawa ya kulevya na baada ya kuyapata waliyauza hayo madawa" alisema Sirro 

Kamanda Sirro aliendelea kusema kuwa mpaka sasa wanawashikilia watu wanne ambayo wamehusika katika jambo hilo.

"Mpaka sasa tunawashikilia watu wanne ambao wanakiri kupasua mwili huo ambao ni wahusika wakuu na ni wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala lakini tumekwenda mbali zaidi baada ya kufanya upasuaji wamemuuzia nani naye amekatwa pia na anaeleza kuwa alinunua hayo madawa, lakini pia naye alichukua na kumuuzia mtu mwingine anayefahamika kwa jina la Ally Nyundo, huyu Nyundo tulishamkataga na kumpeleka kwa Mkemia Mkuu yeye alionekana ni mtumiaji, kimsingi tuna hao watuhumiwa wanne na huyo wa tano aliyekamatwa sasa tunaandaa jalada" alisisitiza Sirro 

HABARI ZAIDI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa January Makamba

Ziara ya Rais Samia Korea kuanza rasmi Mei 31 2024

Bw. Nazar Nicholas (katikati) akikabiziwa tuzo ya WSIS 2024

Tanzania yashinda Tuzo WSIS 2024, nchini Uswisi

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20