MC Piipili akiwa na mchumba wake 'Cute Mena'.
MC Pilipili amesema harusi hiyo inatarajiwa kufanyika baada ya Sikukuu ya Pasaka na itakuwa na kiingilio kitakachoanzia Sh10,000 kwa watu wa kawaida.
Amesema amefikia hatua ya kuweka kiingilio kwa kuwa hadi sasa watu wanaotaka kuhudhuria harusi hiyo ni wengi na ili kutowakosesha wengine haki ya kuiona, ameona ni bora kuweka kiingilio.
”Mpaka ninavyoongea na wewe hapa watu ni wengi sana wanaotamani siku hiyo ifike waweze kushuhudia na mimi nimeona nisiwanyime hiyo nafasi bila kujali uwezo wao kifedha, naamini kiingilio hicho kitawafaa kushiriki nasi na kusherekea siku hiyo muhimu katika maisha yetu na mke wangu mtarajiwa,” amesema.
MC Pilipili alivyoibua gumzo mitandaoni
Januari mwaka huu, mshereheshaji huyo aliibua gumzo mtandaoni baada ya kuonekana akilia wakati wa hafla ya kumvisha pete mchumba wake, Philomena Thadey.