Alhamisi , 18th Sep , 2014

Msanii wa muziki Cindy Sanyu, pamoja na mpenzi wake Ken Muyiisa wameonyesha hatua kuelekea katika kuhalalisha mahusiano haya, hasa baada ya Ken kuamua kujitambulisha rasmi nyumbani kwa msanii huyu mwanzoni mwa wiki.

msanii wa muziki wa nchini Uganda Cinderella Sanyu

Kufuatia hatua, hii aliyekuwa mpenzi wa Ken na mama wa mtoto wake, Phina Mugerwa, ameandika ujumbe wa kuwatakia kila la heri wasanii hawa katika hatua hii mpya ya mahusiano.

Cindy ambaye amekuwa na kiu kubwa ya kuolewa huenda sasa akawa anaikaribua ndoto yake, huku ikielezwa kuwa sababu kubwa ya yeye kuachana na Mario ambaye ni baba wa mwanae, ni hatua ya jamaa huyu kutotaka kumuoa licha ya kuishi pamoja zaidi ya miaka 10.