Msanii na bosi wa lebo ya Konde Gang Harmonize akiwa na msanii wake mpya Young Skales
Harmonize ametangaza hivyo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo siku ya jana Julai 30 alisema leo Julai 31, 2020 atatangaza rasmi kusaini msanii mpya ambaye atajiunga ndani ya lebo hiyo.
Aidha wakati anamtambulisha kwenye lebo hiyo Harmonize ametumia ukurasa huo huo wa Instagram kusema "Ndoto za muziki wa Afrika kwenda duniani, tunayo furaha kumkaribisha msanii Genius kutoka Nigeria kaka yangu Young Skales kwenye familia ya Konde Gang, hii ni timu ya ndoto"
Msanii huyo kutoka nchini Nigeria Young Skales ataungana na msanii mwenziye Ibraah Tz ambao watakuwa pamoja kwenye lebo ya Konde Gang.