Harmonise
Kama utaratibu wetu eNewz ulivyo, kupima joto la kisiasa katika kila kinachoendelea kutoka kwa wasanii na wadau wa burudani, kwa upande wa Harmonise amesema Magufuli anaonesha mwanga na matumaini ambayo yalikuwa yamepotea kwa watanzania wengi, akihusisha suala zima la kusherehekea uhuru kwa kufanya kazi ya usafi, kuundwa kwa baraza dogo la mawaziri kati ya mambo mengine, kitu ambacho ni cha kushukuru Mungu.
Ikiwa leo pia baraza jipya la mawaziri lililotangazwa na Rais Magufuli limeapishwa, kama sehemu ya wanajamii, msanii huyo anayetikisa chati na ngoma ya Aiyola, anaungana na mastaa wengine wengi wa Tanzania, wengine wakichukua hatua ya kutengeneza wimbo kutoa maoni yao mbalimbali kuhusiana na uongozi mpya hapa Tanzania.