Jumanne , 8th Dec , 2015

Kutokana na kutoka kwa rekodi za wasanii kwa wingi zaidi katika kipindi hiki, Ben Pol ameweka wazi mtazamo wake kuwa kiushindani ni sawa kabisa kwa wasanii kufanya hivyo bila kupeana nafasi, ili mwisho wa siku kupata rekodi kali itakayoweza ku 'hit'.

Ben Pol

Licha ya suala hili kuibua maoni tofauti tofauti kutoka kwa watu, Ben Pol amesema kuwa, kazi zikitoka kwa wingi kama hivi, mashabiki wanabaki na kazi ya kuamua ni nani mkali na anaweza kumudu ushindani.

enews haikutaka kumwacha Ben Pol hivihivi, ilitaka kufahamu kutoka kwake, atasimamia vipi maagizo ya Mhe. Rais katika kuadhimisha Uhuru kesho, ambapo ameeleza kuwa atakuwa akifanya usafi katika maeneo ya Tandale sokoni na watu wake wa karibu, akitaka wananchi kutoa ushirikiano katika hilo.

Tags: