Jumatatu , 14th Apr , 2014

Aliyekuwa mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya dansi hapa nchini, Marehemu Maalim Gurumo anatarajiwa kuzikwa siku ya kesho kijijini kwao huko Masaki wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani baada ya kufanyiwa kisomo nyumbani kwake eneo la Mabibo Jijini Dar.

Marehemu Maalim Muhidin Gurumo

Kwa mujibu wa mtoto wa kwanza wa Marehemu, Abdallah Gurumo kwa sasa msiba bado upo Mabibo ambapo jioni ya leo kutafanyika kisomo maalum kwa minajili ya taratibu za dini ya Kiislamu kwa ajili ya marehemu.

Marehemu Gurumo alifariki dunia jana jioni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na maradhi ya moyo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Unaweza kumsikiliza msemaji wa Familia ya Gurumo, Bwana Yahaya Mikole akieleza ratiba nzima ya msiba hapa;