Jumatatu , 1st Dec , 2014

Kutokana na kuwepo kwa uchache wa kolabo za wasanii wa kike hapa Tanzania, Msanii wa muziki Grace Matata, amesema kuwa kwa mtazamo wake hali hii inasababishwa na uchache wa wasanii wa kike katika sekta hiyo na pia kutokufahamiana.

msanii wa muziki wa bongofleva nchini Grace Matata

Grace katika maelezo yake amekanusha mtazamo kuwa, hali hii inachangiwa kutokupendana kwa wasanii wa kike, huku akisisitiza kuwa kwa upande wake kungekuwepo na nafasi, angekwishafanya rekodi za kutosha na wanawake wenzake wanaofanya muziki.