Jumanne , 6th Jan , 2015

Mwanamasumbwi na vilevile msanii wa muziki Golola Moses kutoka nchini Uganda, amefanikiwa kuviteka vichwa vya habari mbalimbali akiwa na tuhuma za kushindwa kulipa kodi kwa miezi 7 sasa katika nyumba aliyopanga huko Mutundwe.

Mwanamasumbwi nyota wa Uganda Moses Golola

Taarifa kuhusiana na hili zimevifikia vyombo vya habari ikiwa ni madai ya mwenye nyumba wa Golola ambaye amedai kuwa mpangaji wake huyo amekuwa akimkwepa akidaiwa kodi tangu mwezi Aprili mwaka jana.

Msanii huyu mpaka sasa hajapatikana kutolea ufafanuzi taarifa hizi tata juu yake.