Jumanne , 16th Apr , 2019

Tasnia ya burudani nchini Tanzania inatarajia kusikia tena muziki mpya wa nguli wa Hip Hop na 'freestyle' aliyeaga dunia hivi karibuni, Golden Jacob (Godzilla).

Kwenye acount yake ambayo inaendeshwa na mmoja wa wana familia, ametoa taarifa kuwa Godzilla aliacha nyimbo zaidi ya mia moja (100) studio, ambazo wataanza kuziachia hivi karibuni.

Taarifa iliyotolewa na acount ya Godzilla

 

 

Godzilla alifariki dunia Februari 13 mwaka huu, baada ya kufariki ghafla, na kuleta simanzi kubwa kwenye tasnia ya burudani nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

Godzilla akiwa studio