Gabo (Katikati) akiwa baada ya kupokea tuzo zake mbili katika EATV Awards
Siri aliyoitoa Gabo umuhimu wa kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kutunga filamu yoyote ili iwe na ujumbe unaoigusa jamii moja moja.
Amesema tatizo kubwa kwa watunzi wa filamu nchini ni kutofanya utafiti wa kutosha kabla ya kuandika story zao.
Gabo alitoa somo hilo mara baada ya kupokea tuzo ya filamu bora ya mwaka kupitia filamu ya "Safari ya Gwalu', katika Tuzo za EATV zilizofanyika mwishoni mwa wiki na kuelezea siri iliyojificha ndani ya filamu hiyo kiasi cha kuwa bora na kutwaa tuzo hizo kubwa Afrika Mashariki.
Msikilize hapa Gabo akiwa mwenye furaha.