
Leakey ambaye ni mtoto wa wanasayansi wa kwanza kugundua fuvu la binadamu nchini Tanzania Dr. Loius na Marry Leakey, amewaambia waandishi wa habari kuwa filamu hiyo itatoa tumaini jipya kwa Nairobi na kuinua sekta ya utalii nchini humo.
"Tutafanya filamu na itatengenezwa Kenya kwa uhakika", alisema Leakey.
Kenya imekuwa ikihamasiha filamu hiyo kumuhusu Leakey, kusherehekea kuokoa wanyama pori toka kwa majangili, wakiwa na matumaini ya kurudisha watalii ambao wamepungua kutokana na mashambulizi ya Al Shabaab kutoka nchi jirani ya Somalia.
Filamu hiyo pia itaiweka Kenya katika rada ya watengena filamu na kusaidia kuokoa biashara ambayo imepotea na kwenda nchini Afrika Kusini, baada ya ya ushindi wa tuzo za Academy wa filamu ya "Out of Africa" iliyofanyika miaka mitatu iliyopita, iliyoandikwa na Karen Blixens wakati wa ukoloni.
Leakey amesema ameshajadili na Anjelina Jolie wiki iliyopita na kwamba muongozo wa filamu hiyo utakuwa tayari baada ya wiki chache kupita, na maandalizi ya kushoot filamu hiyo yataanza mapema mwaka 2016.
Muigizaji wa Hollywood Brad Pitt ambaye ni mume wa Anjelina Jolie, alikuwa kwenye mtazamo wa kucheza kama muhusika mkuu Dr. Leakey, lakini leakey mwenyewe amesema itategemea iwapo ataipenda.