Jumanne , 17th Mar , 2015

Wasanii wa muziki Farid Kubanda (Fid Q) na Khadija Shaban Keysha, pamoja na mchoraji na msanii maarufu Paul Ndunguru wametunukiwa tuzo za heshima sambamba na Watanzania watano mashuhuri kutoka Umoja wa Ulaya.

Msanii wa muziki wa bongofleva nchini Keisha

Wasanii hao wametunukiwa tuzo hizo maarufu kutokana na mchango wa kila mmoja wao katika kuwaletea Watanzania maendeleo.

Tuzo hizo zimetolewa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwaka wa maendeleo kwa nchi za Ulaya ambayo hujulikana kwa kifupi kama EYD ambapo msanii wa muziki Keisha amesisitiza kuwa, kilichochangia yeye kupata tuzo hiyo mbali na shughuli zake ni kujiheshimu, wakati kwa upande wa Fid Q, suala zima la ukarimu na kusaidia vijana likiwa limembeba.