Jumatano , 27th Mar , 2019

Msanii wa kizazi kipya anayesumbua kwa sasa na ngoma 'You are the best', Ommy Dimpoz amesema kwa sasa yupo kwenye mchujo mkali sana wa kuweza kumpata mwanamke wa kuoa ambaye ataweza kumtunza.

Ommy Dimpoz

Akipiga story na www.eatv.tv, Ommy amesema kutokana na kwamba marafiki zake karibu wote wana familia yeye anapambana kupata mwanamke ambaye anauwezo wa kumtunza kutokana na afya yake.

Anasema anahitaji mwanamke anayejua kupika uji supu na hata kumjali mgonjwa kwa kila hali kutokana na kwamba yeye siyo mzima sana.

"Unaweza kuangukia kwa 'Slay Queen' hajui hata kuandaa chakula cha mgonjwa itakuwa ni shida. Kwa sasa yaani nina chuja sana", amesema.

Akizungumzia mahusiano yake ya kikazi yeye pamoja na Meneja wake Seven Mosha, Ommy anasema hajawahi kugombana na meneja wake kwa kuwa amekuwa familia yake.

"Seven ni mtu wa karibu sana, hatuwezi kugombana. Tuko karibu sana ndiyo maana hata wakati naumwa aliweza kuacha shughuli zote na kuja kuniuguza.  Ni zaidi ya meneja nisipoongea nae siku mbili nahisi kuumwa. Familia yetu yenyewe ni ndogo sana ndiyo maana hata kukitokea jambo tunaweza kutatua".

Kuhusu ukaribu wake na Msanii  AY, kama anaweza kumshawishi na yeye kuoa nchini Rwanda, Ommy amesema yeye atabaki nyumbani kwa kuwa alisha ahidi.

"Mimi sitakwenda nje, Mimi ni wenu tuu...Haijalishi ni mkoa gani lakini mimi nitaoa nyumbani", ameongeza msanii huyo.

Ngoma mpya ya Dimpoz imekuja mwezi mmoja baada ya kutoa wimbo wa 'Ni wewe' alioutoa kwa ajili ya kumtukuza Mungu kutokana na kumponya ugonjwa uliomuweka kitandani kwa muda mrefu.

Mtazame hapa chini akizungumza