Jumapili , 15th Sep , 2024

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, amesema mpango wao wa kufanya maandamano septemba 23 uko palepale.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu

 

Amesema hayo leo Septemba 15, 2024, baada ya kushiriki kongamano la tano la kitaifa la Ekaristi Takatifu katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo amesema msimamo wao ni ule ule kufanya maandamano.

"Msimao wetu ni kwamba tutafuata kile ambacho sheria yetu inataka na sheria zinasema ni haki kufanya maandamano na ni haki kupatiwa ulinzi wakati wa maandamano," amesema Lissu