msanii wa muziki wa nchini Uganda Desire Luzinda
Desire katika waraka mfupi wa msamaha alioandika, amewataka radhi mama yake mzazi, mwanae wa kike, familia yake marafiki na mashabiki wake na kuwataka kufahamu kuwa, kuvuja kwa picha hizi kumetokana na kuvunjika kwa uaminifu kutoka kwa mtu aliyempenda akiwa na nia ya kutaka kumharibia maisha sasa.
Msanii huyu amesema kuwa, anakubali kubeba lawama zote kutokana na tukio hili la aibu huku akiwaweka wazi kuwa, juhudi zinazofanyika na vyombo vya usalama kuhakikisha kuwa haki inatendeka katika hili.