Jumapili , 15th Feb , 2015

Star wa muziki Dayna Nyange amekanusha uvumi ulioenea mtaani kuwa ngoma yake iliyovuja inayokwenda kwa jina Pepea ni rekodi ambayo ameamua kuitoa kwa kukusudia hasa kutokana na hali halisi anayopitia sasa ya kutendwa katika mahusiano yake.

Dayna

Dayna amesisitiza kuwa Pepea ni ngoma ambayo hakuwa amefikiria kuutoa rasmi, akiwa na mpango wa kuifanyia marekebisho kutokana na kukaa muda mrefu, na kuwataka mashabiki wake kukaa tayari kwa ujio wake rasmi mwishoni mwa mwezi huu, na hapa Dayna anaeleza ilikuwaje.