Jumatatu , 5th Feb , 2024

Wazee kubeti wanajua maana ya mkeka/mikeka kuchanika kwa sababu ni jambo ambalo hawataki liwatokee kabisa ndio hivyohivyo huenda mashabiki wa Burna Boy na Davido hawataki kusikia story za wasanii hao kukosa tuzo za Grammy 2024.

Kulia picha ya Davido kulia na Burna Boy kushoto

Burna Boy na Davido wametoka patupu licha ya kuwa wasanii wa Africa waliotajwa kwenye category ya tuzo za Grammy 2024.

BurnaBoy ametajwa katika vipengele vinne ambavyo ni Global Music Album, African Music Performance, Global Music Performance na Melodic Rap Performance.

Na Davido alikuwa katika vipengele vitatu Global Music Album, African Music Performance, Global Music Performance.