Msanii Davido wa Nigeria
Davido ametwaa tuzo mbili zikiwemo za msanii bora wa kiume na msanii bora wa mwaka ambapo katika sherehe hizo pia kundi la Mafikizolo limetwaa tuzo ya kundi bora la mwaka.
Aidha msanii Tiwa Savage wa nchini Nigeria ametwaa tuzo ya msanii bora wa kike, ambapo Lupita Nyong'o amezidi kung'arisha nyota yake kwa tuzo ya Personality of the Year, huku Ashish J. Thakkar kutoka Tanzania akitwaa tuzo ya Best Leadership Award.